Isaiah 6:8
Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu?” Nami nikasema, “Mimi hapa. Nitume mimi!”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 3:8Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani.
Genesis 11:7Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
Genesis 22:11Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!” Akajibu, “Mimi hapa.”
Deuteronomy 4:33Je, kuna watu wengine wowote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi?
1 Kings 22:20Naye Bwana akasema, ‘Ni nani atakayemshawishi Ahabu ili aishambulie Ramoth-Gileadi na kukiendea kifo chake huko?’ “Mmoja akapendekeza hili na mwingine lile.
Ezekiel 1:24Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi, + 1:24 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao.