Isaiah 60:2
Tazama, giza litaifunika dunia 2 na giza kuu litayafunika mataifa, 1 lakini Bwana atazuka juu yako 2 na utukufu wake utaonekana juu yako. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
1“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja 2 na utukufu wa Bwana umezuka juu yako. 1
3Mataifa watakuja kwenye nuru yako 2 na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako. 1
Cross References
Leviticus 9:23Kisha Mose na Aroni wakaingia kwenye Hema la Kukutania. Walipotoka nje, wakawabariki watu. Nao utukufu wa Bwana ukawatokea watu wote.
1 Kings 8:11Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu lake.
Isaiah 8:22Kisha wataangalia duniani na kuona tu dhiki na giza, hofu na huzuni tupu, nao watasukumiwa kwenye giza nene kabisa.
Isaiah 62:1Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, 2 kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, 1 mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko, 2 wokovu wake kama mwanga wa moto. 1
Ezekiel 10:4Kisha utukufu wa Bwana ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mngʼao wa utukufu wa Bwana.
Haggai 2:7Nitatikisa mataifa yote, nacho kile kinachotamaniwa na mataifa yote kitakuja, nami nitaujaza utukufu katika nyumba hii,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.