Isaiah 7:3
Ndipo Bwana akamwambia Isaya, “Toka uende, wewe na mwanao Shear-Yashubu, + 7:3 Shear-Yashubu maana yake Mabaki Watarudi. mkutane na Ahazi huko mwisho wa mfereji wa Bwawa la Juu, kwenye barabara iendayo Shamba la Dobi.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 7:15Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka.
2 Kings 18:17Mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wake mkuu, na afisa wake mkuu, na jemadari wa jeshi, pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Wakaja Yerusalemu na kusimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Isaiah 6:13Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi, 2 itaharibiwa tena. 1 Lakini kama vile mvinje na mwaloni 2 ibakizavyo visiki inapokatwa, 2 ndivyo mbegu takatifu 2 itakavyokuwa kisiki katika nchi.”
Isaiah 22:10Mlihesabu majengo katika Yerusalemu 2 nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta. 1
Isaiah 36:2Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Jeremiah 19:2na mtoke mwende mpaka kwenye Bonde la Ben-Hinomu, karibu na ingilio la Lango la Vigae. Huko tangaza maneno ninayokuambia,