Yeremia 6:1
“Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini! 2 Kimbieni kutoka Yerusalemu! 1 Pigeni tarumbeta katika Tekoa! 2 Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu! 1 Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini, 2 na uharibifu wa kutisha. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
2Nitamwangamiza Binti Sayuni, 2 aliye mzuri sana na mwororo. 1
Cross References
Joshua 15:63Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, waliokuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.
Joshua 18:28Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake.
2 Samuel 14:2Kwa hiyo Yoabu akamtuma mtu fulani kwenda Tekoa na kumleta mwanamke mwenye hekima kutoka huko. Akamwambia huyo mwanamke, “Jifanye uko katika maombolezo. Vaa nguo za kuomboleza, nawe usitumie mafuta yoyote ya uzuri, jifanye kama mwanamke ambaye amekuwa na huzuni kwa siku nyingi kwa ajili ya kufiwa.
Nehemiah 3:5Sehemu iliyofuatia ilikarabatiwa na watu kutoka Tekoa, lakini wakuu wao walikataa kufanya kazi chini ya wasimamizi wao.
Jeremiah 1:14Bwana akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi.
Jeremiah 4:19Ee mtima wangu, mtima wangu! 2 Ninagaagaa kwa maumivu. 1 Ee maumivu makuu ya moyo wangu! 2 Moyo wangu umefadhaika ndani yangu, 2 siwezi kunyamaza. 1 Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta, 2 nimesikia kelele ya vita. 1