Jeremiah 7:13
Mlipokuwa mnafanya yote haya, asema Bwana, nilisema nanyi tena na tena, lakini hamkusikiliza; niliwaita, lakini hamkujibu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Nehemiah 9:29“Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.
Isaiah 50:2Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja? 2 Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu? 1 Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa? 2 Je, mimi sina nguvu za kukuokoa? 1 Kwa kukemea tu naikausha bahari, 2 naigeuza mito ya maji kuwa jangwa; 1 samaki wake wanaoza kwa kukosa maji 2 na kufa kwa ajili ya kiu. 1
Isaiah 66:4Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali, 2 nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa. 1 Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu, 2 niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza. 1 Walifanya maovu machoni pangu 2 na kuchagua lile linalonichukiza.” 1
Jeremiah 6:10Niseme na nani na kumpa onyo? 2 Ni nani atakayenisikiliza mimi? 1 Masikio yao yameziba, + 6:10 Masikio yameziba kwa Kiebrania ina maana kwamba masikio yao hayajatahiriwa. 2 kwa hiyo hawawezi kusikia. 1 Neno la Bwana ni chukizo kwao, 2 hawalifurahii. 1
Jeremiah 11:7Tangu wakati ule niliwapandisha baba zenu kutoka Misri mpaka leo, niliwaonya tena na tena, nikisema “Nitiini mimi.”
Jeremiah 13:10Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mkanda huu ambao haufai kabisa!