Job 2:3
Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 6:9Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
Job 1:1Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.
Job 1:8Ndipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”
Job 1:21na kusema: 1 “Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi, 2 nami nitaondoka uchi, + 1:21 Au: nitarudi huko uchi. 1 Bwana alinipa, naye Bwana ameviondoa, 2 jina la Bwana litukuzwe.”
Job 9:20Hata kama sikuwa na hatia, kinywa changu kingenihukumu; 2 kama sikuwa na kosa, kingenitangaza kuwa mwenye hatia. 1
Job 27:5Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi; 2 hadi nife, sitakana uadilifu wangu. 1