Waamuzi 1:27
Lakini Manase hawakuwafukuza watu wa Beth-Shani na vijiji vyake, au watu wa Taanaki na vijiji vyake, au watu wa Dori na vijiji vyake, au watu wa Ibleamu na vijiji vyake, au watu wa Megido na vijiji vyake, lakini Wakanaani waliazimu kuishi katika nchi ile.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 23:32Usifanye agano lolote nao wala na miungu yao.
Joshua 17:11Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, + 17:11 Ndiyo Nafoth-Dori. Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi).
Judges 1:1Baada ya kifo cha Yoshua, Waisraeli wakamuuliza Bwana, “Ni nani atakayetangulia kupanda mbele yetu kwa ajili ya kupigana na Wakanaani?”
Judges 5:19“Wafalme walikuja na kufanya vita; 2 wafalme wa Kanaani walipigana 2 huko Taanaki karibu na maji ya Megido, 2 lakini hawakuchukua fedha wala nyara. 1
1 Samuel 31:10Wakaweka silaha zake katika hekalu la Maashtorethi, na kukifunga kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-Shani.
2 Kings 23:29Yosia alipokuwa mfalme, Farao Neko mfalme wa Misri akapanda mpaka Mto Frati kumsaidia mfalme wa Ashuru. Mfalme Yosia akatoka kwenda kupigana naye, lakini Neko akamkabili na kumuua huko Megido.