Waamuzi 18:28
Hapakuwa na yeyote wa kuwaokoa, kwa kuwa kulikuwa mbali sana na Sidoni na hawakuwa na ushirikiano na mtu mwingine yeyote. Mji ulikuwa kwenye bonde karibu na Beth-Rehobu. Wadani wakaujenga upya huo mji na kuishi humo.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Numbers 13:21Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.
Joshua 19:28Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.
Judges 18:7Basi hao watu watano wakaondoka na kufika Laishi, mahali ambapo waliwakuta watu wanaishi salama, kama Wasidoni, kwa utulivu na bila mashaka. Nchi yao haikupungukiwa na kitu chochote, hivyo wakawa tajiri. Pia walikaa mbali sana na Wasidoni, wala hawakushughulika na mtu yeyote.
2 Samuel 14:6Mimi mtumishi wako nilikuwa na wana wawili. Wakapigana wao kwa wao huko shambani wala huko hapakuwa na mtu hata mmoja wa kuwaamua. Mmoja akampiga mwenzake na kumuua.
Psalms 7:2la sivyo watanirarua kama simba 2 na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. 1
Isaiah 23:4Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, 2 kwa kuwa bahari imesema: 1 “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, 2 wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.” 1