Waamuzi 20:41
Ndipo watu wa Israeli wakawageukia, nao Wabenyamini wakatiwa hofu, kwa kuwa walitambua kwamba maafa yamewajia.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Joshua 8:20Watu wa Ai wakaangalia nyuma, wakauona moshi wa huo mji ukielekea angani lakini hawakuwa na nafasi ya kutoroka kwa upande wowote, kwa kuwa wale Waisraeli waliokuwa wanawakimbia kuelekea jangwani walikuwa wamegeuka nyuma kuwakabili wakimbizaji wao.
Isaiah 33:14Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, 2 kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: 1 “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? 2 Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?” 1
Luke 21:26Watu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za angani zitatikisika.
2 Peter 2:12Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiyoyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawaliwa na hisia za mwili, waliozaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa. Hawa nao kama wanyama wataangamizwa pia.
Revelation 18:8Kwa hiyo mapigo yatampata kwa siku moja: 2 mauti, maombolezo na njaa. 1 Naye atateketezwa kwa moto, 2 kwa maana Bwana Mungu amhukumuye ana nguvu.