Lamentations 1:3
Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili, 2 Yuda amekwenda uhamishoni. 1 Anakaa miongoni mwa mataifa, 2 hapati mahali pa kupumzika. 1 Wote ambao wanamsaka wamemkamata 2 katikati ya dhiki yake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:36“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza.
Deuteronomy 28:64Kisha Bwana atawatawanya miongoni mwa mataifa yote, kutoka mwisho mmoja wa dunia hadi mwingine. Huko mtaabudu miungu mingine, miungu ya miti na ya mawe, ambayo ninyi wala baba zenu hamkuijua.
2 Kings 24:14Akawachukua watu wa Yerusalemu wote kwenda uhamishoni: yaani maafisa wote na mashujaa, watu wenye ustadi na ufundi, jumla yao watu elfu kumi. Watu maskini sana ndio tu waliobaki katika nchi.
2 Kings 25:21Huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, mfalme wa Babeli akaamuru wanyongwe. Hivyo Yuda wakaenda utumwani, mbali na nchi yao.
Jeremiah 13:19Miji iliyoko Negebu itafungwa, 2 wala hapatakuwa na mtu wa kuifungua. 1 Watu wa Yuda wote watapelekwa uhamishoni, 2 wakichukuliwa kabisa waende mbali. 1
Jeremiah 24:9Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, popote nitakapowafukuzia.