Maombolezo 1:7
Katika siku za mateso yake na kutangatanga, 2 Yerusalemu hukumbuka hazina zote 2 ambazo zilikuwa zake siku za kale. 1 Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui, 2 hapakuwepo na yeyote wa kumsaidia. 1 Watesi wake walimtazama 2 na kumcheka katika maangamizi yake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 4:34Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayo Bwana Mungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?
Job 29:2“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, 2 zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda, 1
Psalms 77:3Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; 2 nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. 1
Psalms 79:4Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu, 2 cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. 1
Psalms 147:19Amemfunulia Yakobo neno lake, 2 sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. 1
Isaiah 64:10Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa; 2 hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa. 1