Lamentations 2:9
Malango yake yamezama ardhini, 2 makomeo yake ameyavunja na kuyaharibu. 1 Mfalme wake na wakuu wake wamepelekwa uhamishoni 2 miongoni mwa mataifa, 2 sheria haipo tena, 1 na manabii wake hawapati tena 2 maono kutoka kwa Bwana. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 28:36Bwana atakupeleka wewe na mfalme uliyemweka juu yako uende kwenye taifa ambalo hukulijua wewe wala baba zako. Huko utaabudu miungu mingine, miungu ya miti na mawe.
1 Samuel 28:6Ndipo Sauli akauliza ushauri kwa Bwana, lakini Bwana hakumjibu kwa ndoto, wala kwa Urimu, + 28:6 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. wala kwa njia ya manabii.
2 Kings 25:7Wakawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake. Kisha wakayangʼoa macho yake, wakamfunga kwa pingu za shaba na kumpeleka Babeli.
Nehemiah 1:3Wakaniambia, “Wale walionusurika kwenda uhamishoni, wale ambao wamerudi kwenye lile jimbo, wako katika taabu kubwa na aibu. Ukuta wa Yerusalemu umebomoka, na malango yake yamechomwa moto.”
Isaiah 24:12Mji umeachwa katika uharibifu, 2 lango lake limevunjwa vipande. 1
Jeremiah 39:2Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia, ukuta wa mji ulibomolewa.