Lamentations 4:13
Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake, 2 na maovu ya makuhani wake, 1 waliomwaga ndani yake 2 damu ya wenye haki. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Jeremiah 2:20“Zamani nilivunja nira yako 2 na kukatilia mbali vifungo vyako; 2 ukasema, ‘Sitakutumikia!’ 1 Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu 2 na chini ya kila mti uliotanda matawi yake 2 ulijilaza kama kahaba. 1
Jeremiah 6:13“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa, 2 wote wana tamaa ya kupata faida zaidi; 1 manabii na makuhani wanafanana, 2 wote wanafanya udanganyifu. 1
Jeremiah 23:11“Nabii na kuhani wote si wacha Mungu; 2 hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,” 4 asema Bwana. 1
Lamentations 2:14Maono ya manabii wako 2 yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, 1 hawakuifunua dhambi yako 2 ili kukuzuilia kwenda utumwani. 1 Maneno waliyokupa 2 yalikuwa ya uongo na ya kupotosha. 1
Ezekiel 22:25Kuna hila mbaya ya wakuu ndani yake kama simba angurumaye akirarua mawindo yake, wanakula watu, wanachukua hazina na vitu vya thamani na kuongeza idadi ya wajane ndani yake.
Ezekiel 22:27Maafisa wake walioko ndani yake ni kama mbwa mwitu wararuao mawindo yao, wanamwaga damu na kuua watu ili kupata faida ya udhalimu.