Lamentations 2:14
Maono ya manabii wako 2 yalikuwa ya uongo na yasiyofaa kitu, 1 hawakuifunua dhambi yako 2 ili kukuzuilia kwenda utumwani. 1 Maneno waliyokupa 2 yalikuwa ya uongo na ya kupotosha. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 9:15Wazee na watu mashuhuri ndio vichwa, 2 nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia. 1
Jeremiah 2:8Makuhani hawakuuliza, 2 ‘Yuko wapi Bwana?’ 1 Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; 2 viongozi waliasi dhidi yangu. 1 Manabii walitabiri kwa jina la Baali, 2 wakifuata sanamu zisizofaa. 1
Jeremiah 6:13“Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa, 2 wote wana tamaa ya kupata faida zaidi; 1 manabii na makuhani wanafanana, 2 wote wanafanya udanganyifu. 1
Jeremiah 14:13Lakini nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’ ”
Jeremiah 23:22Lakini kama wangesimama barazani mwangu, 2 wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu, 1 nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya 2 na kutoka matendo yao maovu.” 1
Jeremiah 23:31“Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘ Bwana asema.’