Lamentations 4:7
Wakuu wao walikuwa wamengʼaa kuliko theluji 2 na weupe kuliko maziwa, 1 miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, 2 kuonekana kwao kama yakuti samawi. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Judges 13:5kwa kuwa utachukua mimba na utamzaa mtoto mwanaume. Wembe usipite kichwani pake, kwa kuwa huyo mwana atakuwa Mnadhiri wa Mungu, aliyewekwa wakfu kwa ajili ya Mungu tangu tumboni mwa mama yake, naye ataanza kuwaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti.”
Judges 16:17Hivyo akamwambia yule mwanamke siri yake yote, akamwambia, “Wembe haujapita kamwe kichwani mwangu, kwa kuwa mimi ni Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni mwa mama yangu. Kama nywele za kichwa changu zikinyolewa, nguvu zangu zitanitoka, na nitakuwa dhaifu kama mtu mwingine yeyote!”
Psalms 51:7Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, 2 unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. 1
Song of Solomon 5:10Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu, 2 wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu. 1
Daniel 1:15Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko yeyote kati ya wale vijana waliokula chakula cha mfalme.
Luke 1:15Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Bwana, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji chochote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake.