Walawi 14:10
“Siku ya nane, ni lazima alete kondoo dume wawili na kondoo jike mmoja, wote wa mwaka mmoja na wasio na dosari, pamoja na sehemu tatu za kumi za efa + 14:10 Sehemu tatu za kumi za efa ni sawa na kilo 3. za unga laini uliochanganywa na mafuta, kwa ajili ya sadaka ya nafaka, na logi moja + 14:10 Logi ni kipimo cha ujazo ambacho ni sawa na lita 0.3. ya mafuta.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 29:40Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja + 29:40 Efa moja ni sawa na kilo 22. ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini + 29:40 Robo ya hini ni sawa na lita moja. ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.
Leviticus 1:10“ ‘Kama sadaka ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la kondoo au mbuzi, atamtoa mnyama dume asiye na dosari.
Leviticus 2:11“ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto.
Leviticus 4:32“ ‘Ikiwa ataleta mwana-kondoo kama sadaka yake ya dhambi, atamleta jike asiye na dosari.
Leviticus 14:12“Kisha kuhani atamchukua mmoja wa wale kondoo dume na kumtoa kuwa sadaka ya hatia, pamoja na ile logi moja ya mafuta; ataviinua mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.
Leviticus 14:21“Hata hivyo, kama ni maskini na hawezi kupata vitu hivi, lazima achukue mwana-kondoo mmoja kama sadaka ya hatia ipate kuinuliwa ili kumfanyia upatanisho, pamoja na sehemu ya kumi ya efa + 14:21 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na lita 2. ya unga laini uliochanganywa na logi moja ya mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka,