Leviticus 7:35
Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, ambazo zilitengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu ili kumtumikia Bwana katika kazi ya ukuhani.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 28:1“Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Exodus 29:7Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake.
Exodus 40:13Kisha mvike Aroni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani.
Leviticus 8:30Kisha Mose akachukua sehemu ya mafuta ya upako, na sehemu ya damu kutoka kwenye madhabahu, na kuvinyunyiza juu ya Aroni na mavazi yake, na juu ya wanawe na mavazi yao. Kwa hiyo akamweka Aroni na mavazi yake wakfu, pamoja na wanawe na mavazi yao.
Numbers 18:8Kisha Bwana akamwambia Aroni, “Mimi mwenyewe nimekuweka kuwa mwangalizi wa sadaka zote zitakazotolewa kwangu; matoleo yote matakatifu Waisraeli wanayonipa ninakupa wewe na wanao kama sehemu yenu na fungu lenu la kawaida.
Isaiah 61:1Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu, 2 kwa sababu Bwana amenitia mafuta 2 kuwahubiria maskini habari njema. 1 Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, 2 kuwatangazia mateka uhuru wao, 1 na hao waliofungwa 2 habari za kufunguliwa kwao; 1