Luke 6:35
Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
36Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. 1 Kuwahukumu Wengine (Mathayo 7:1-5)
Cross References
Leviticus 25:35“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie kama vile ambavyo ungelimsaidia mgeni au kama mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi katikati yako.
Psalms 112:5Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, 2 anayefanya mambo yake kwa haki. 1
Proverbs 19:17Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, 2 naye atamtuza kwa aliyotenda. 1
Matthew 5:44Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi,
Luke 1:32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.
John 13:35Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”