Luke 9:3
Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
2kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
4Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
Cross References
Psalms 37:3Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; 2 Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. 1
Mark 6:8Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu.
Luke 5:29Kisha Lawi akamfanyia Yesu karamu kubwa nyumbani kwake, nao umati mkubwa wa watoza ushuru na watu wengine walikuwa wakila pamoja nao.
Luke 12:22Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake: “Kwa hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu kwamba mtakula nini; au msumbukie miili yenu kwamba mtavaa nini.
Luke 22:35Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma bila mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu chochote?” Wakajibu, “La, hatukupungukiwa na kitu chochote.”