Mark 4:27
Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
26Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.
28Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke.
Cross References
Ecclesiastes 8:17ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna yeyote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.
John 3:7Kwa hiyo usishangae ninapokuambia huna budi ‘kuzaliwa mara ya pili.’
2 Thessalonians 1:3Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.