Mathayo 11:29
Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
28“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
30Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”
Cross References
2 Chronicles 10:11Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi; mimi nitawachapa kwa nge.’ ”
Isaiah 42:1“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, 2 mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; 1 nitaweka Roho yangu juu yake, 2 naye ataleta haki kwa mataifa. 1
Zechariah 9:9Shangilia sana, ee Binti Sayuni! 2 Piga kelele, Binti Yerusalemu! 1 Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, 2 ni mwenye haki, naye ana wokovu, 2 ni mpole, naye amepanda punda, 2 mwana-punda, mtoto wa punda. 1
Matthew 11:27“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia. 1 Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo
Matthew 17:5Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililongʼaa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.”
Matthew 28:20nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.”