Matthew 19:22
Yule kijana aliposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi. 1 Hatari Za Utajiri
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
But when the young man heard that saying, he went away sorrowful: for he had great possessions.
In Context
Cross References
Psalms 17:14Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, 2 kutokana na watu wa ulimwengu huu 2 ambao fungu lao liko katika maisha haya. 1 Na wapate adhabu ya kuwatosha. 2 Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, 2 hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. 1
Daniel 6:14Wakati mfalme aliposikia hili, akahuzunika mno. Akakusudia kumwokoa Danieli, hivyo akafanya kila jitihada ya kumwokoa hadi jua likatua.
Matthew 13:22Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.
Matthew 16:26Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Mark 10:22Yule mtu aliposikia hayo, akasikitika sana. Akaondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
John 19:12Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, “Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu yeyote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari.”