Matthew 19:21
Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
20Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?”
Cross References
Genesis 6:9Hivi ndivyo vizazi vya Noa. Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
Job 1:1Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.
Matthew 4:19Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”
Matthew 5:48Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Matthew 8:22Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.” 1 Yesu Atuliza Dhoruba (Marko 4:35-41; Luka 8:22-25)
Matthew 16:24Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.