Matthew 22:10
Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
9Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’
Cross References
Matthew 13:38Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu.
Matthew 22:11“Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi.
Matthew 25:10“Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
2 Corinthians 12:21Nina hofu kwamba nitakapokuja tena kwenu, Mungu wangu atanidhili mbele yenu, nami nitasikitishwa na wengi waliotenda dhambi mbeleni, na wala hawajatubu kwa uchafu wao, uasherati, na ufisadi walioushiriki.
Revelation 2:14“Hata hivyo, nina mambo machache dhidi yako: Unao watu wafuatao mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa kafara kwa sanamu na kufanya uasherati.
Revelation 5:9Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema: 1 “Wewe unastahili kukitwaa kitabu 2 na kuzivunja lakiri zake, 1 kwa sababu ulichinjwa 2 na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu 1 kutoka kila kabila, kila lugha, 2 kila jamaa na kila taifa. 1