Matthew 4:10
Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
9kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.”
Cross References
Deuteronomy 6:13Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake.
Joshua 24:14“Sasa basi mcheni Bwana na kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ngʼambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieni Bwana.
1 Chronicles 21:1Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli.
Job 1:12Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.” Ndipo Shetani akatoka mbele za Bwana.
Psalms 109:6Agiza mtu mwovu ampinge, 2 mshtaki + 109:6 Mshtaki hapa maana yake ni Shetani. asimame mkono wake wa kuume. 1
Matthew 16:23Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”