Micah 1:4
Milima inayeyuka chini yake 2 na mabonde yanagawanyika 1 kama nta mbele ya moto, 2 kama maji yatiririkayo kasi 2 kwenye mteremko. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Judges 5:4“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, 2 ulipopita katika mashamba ya Edomu, 1 nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, 2 naam, mawingu yakamwaga maji. 1
Psalms 97:5Milima huyeyuka kama nta mbele za Bwana, 2 mbele za Bwana wa dunia yote. 1
Amos 9:5Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, 2 na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: 1 nayo nchi yote huinuka kama Naili, 2 kisha hushuka kama mto wa Misri; 1
Habakkuk 3:6Alisimama, akaitikisa dunia; 2 alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. 1 Milima ya zamani iligeuka mavumbi 2 na vilima vilivyozeeka vikaanguka. 2 Njia zake ni za milele. 1
Zechariah 14:4Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.
Revelation 20:11Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana.