Micah 3:6
Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono, 2 na giza, msiweze kubashiri. 1 Jua litawachwea manabii hao, 2 nao mchana utakuwa giza kwao. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 74:9Hatukupewa ishara za miujiza; 2 hakuna manabii waliobaki, 1 hakuna yeyote kati yetu ajuaye 2 hali hii itachukua muda gani. 1
Isaiah 29:10Bwana amewaleteeni usingizi mzito: 2 Ameziba macho yenu (ninyi manabii); 2 amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji).
Jeremiah 13:16Mpeni utukufu Bwana Mungu wenu, 2 kabla hajaleta giza, 1 kabla miguu yenu haijajikwaa 2 juu ya vilima vitakavyotiwa giza. 1 Mlitarajia nuru, 2 lakini ataifanya kuwa giza nene 2 na kuibadili kuwa huzuni kubwa. 1
Jeremiah 18:18Wakasema, “Njooni, tutunge hila dhidi ya Yeremia; kwa kuwa kufundisha sheria kwa kuhani hakutapotea, wala shauri litokalo kwa mwenye hekima, wala neno la manabii. Hivyo njooni, tumshambulie kwa ndimi zetu na tusijali chochote asemacho.” 1
Ezekiel 13:9Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.
Ezekiel 13:23kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”