Nahumu 1:3
Bwana si mwepesi wa hasira naye ni mwenye nguvu, 2 Bwana hataacha kuadhibu wenye hatia. 1 Njia yake ipo katika kisulisuli na tufani, 2 na mawingu ni vumbi la miguu yake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 19:16Asubuhi ya siku ya tatu kulikuwa na ngurumo na radi pamoja na wingu nene juu ya mlima na mlio mkubwa sana wa tarumbeta. Kila mmoja aliyekuwa kambini akatetemeka.
Numbers 14:18‘ Bwana si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’
1 Kings 19:11Bwana akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Bwana, kwa kuwa Bwana yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Bwana, lakini Bwana hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini Bwana hakuwamo kwenye lile tetemeko.
Job 9:4Hekima yake ni kubwa sana na ana uwezo mwingi mno. 2 Ni nani aliyempinga naye akawa salama? 1
Job 38:1Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: 1
Psalms 50:3Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, 2 moto uteketezao unamtangulia, 2 akiwa amezungukwa na tufani kali. 1