Nehemia 1:10
“Hawa ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa nguvu zako kuu na mkono wako wenye nguvu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 6:1Kisha Bwana akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”
Exodus 13:3Ndipo Mose akawaambia watu, “Ikumbukeni siku hii, siku ambayo mlitoka katika nchi ya Misri, katika nchi ya utumwa, kwa sababu Bwana aliwatoa humo kwa mkono wenye nguvu. Msile chochote kilichotiwa chachu.
Exodus 13:14“Katika siku zijazo, mwanao akikuuliza, ‘Hii ina maana gani?’ Mwambie, ‘Kwa mkono wenye nguvu Bwana alitutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
Exodus 15:13“Katika upendo wako usiokoma utawaongoza 2 watu uliowakomboa. 1 Katika nguvu zako utawaongoza 2 mpaka makao yako matakatifu. 1
Deuteronomy 9:29Bali wao ni watu wako, urithi wako ule ulioutoa Misri kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyooka.”
Psalms 74:2Kumbuka watu uliowanunua zamani, 2 kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: 2 Mlima Sayuni, ambamo uliishi. 1