Nehemia 10:28
“Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu, + 10:28 Yaani Wanethini . na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Sheria ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 20:24Lakini niliwaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, ambaye amewatenga kutoka mataifa.
Ezra 2:70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.
Ezra 10:11Sasa tubuni kwa Bwana, Mungu wa baba zenu mkafanye mapenzi yake. Jitengeni na mataifa wanaowazunguka na wake zenu wa kigeni.”
Nehemiah 8:2Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba, kuhani Ezra akaleta Sheria mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwamo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.
Nehemiah 13:3Watu waliposikia sheria hii, waliwatenga watu wote wasio Waisraeli waliokuwa wa uzao wa kigeni.
Ecclesiastes 5:2Usiwe mwepesi kuzungumza, 2 usiwe na haraka katika moyo wako 2 kuzungumza lolote mbele za Mungu. 1 Mungu yuko mbinguni 2 nawe uko duniani, 1 kwa hiyo maneno yako 2 na yawe machache. 1