Numbers 11:12
Je, watu hawa wote mimi ndiye niliyewatungisha mimba? Je, ni mimi niliyewazaa? Kwa nini unaniambia niwachukue mikononi mwangu, kama vile mlezi abebavyo mtoto mchanga, hadi kwenye nchi uliyowaahidi baba zao?
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
13Nitapata wapi nyama kwa ajili ya watu wote hawa? Wanaendelea kunililia wakisema, ‘Tupe nyama tule!’
Cross References
Genesis 13:15Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele.
Genesis 26:3Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.
Exodus 6:8Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Bwana.’ ”
Deuteronomy 1:31na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Bwana Mungu wenu alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea mpaka mkafika mahali hapa.”
Isaiah 49:15“Je, mama aweza kumsahau mtoto 2 aliyeko matitini mwake akinyonya, 1 wala asiwe na huruma 2 juu ya mtoto aliyemzaa? 1 Ingawa anaweza kusahau, 2 mimi sitakusahau wewe! 1
Ezekiel 34:23Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao.