Numbers 15:5
Pamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 29:40Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja + 29:40 Efa moja ni sawa na kilo 22. ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini + 29:40 Robo ya hini ni sawa na lita moja. ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.
Numbers 28:7Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu.
Judges 9:13“Lakini mzabibu ukaijibu, ‘Je, niache kutoa divai yangu inayofurahisha miungu na wanadamu ili nikawe juu ya miti?’
Ezra 7:17Hakikisha kwamba fedha hizi zimetumika kununua mafahali, kondoo dume na wana-kondoo pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, uvitoe dhabihu juu ya madhabahu ya Hekalu la Mungu wenu katika Yerusalemu.
Song of Solomon 1:4Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! 1 Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki 1 Tunakushangilia na kukufurahia, 1 tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa 1 Tazama jinsi ilivyo bora wakupende! 1
Matthew 26:28Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.