Numbers 24:20
Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake: 1 “Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa, 2 lakini mwisho wake itaangamizwa milele.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 17:8Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu.
Exodus 17:16Mose akasema, “Kwa maana mikono iliinuliwa mpaka kwenye kiti cha enzi cha Bwana. Bwana atakuwa na vita dhidi ya Waamaleki kutoka kizazi hata kizazi.”
1 Samuel 14:48Akapigana kishujaa na kuwashinda Waamaleki, akiikomboa Israeli kutoka mikono ya wale waliokuwa wamewateka nyara. 1 Jamaa Ya Sauli
1 Samuel 27:8Basi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia iteremkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.)
1 Samuel 30:17Daudi akapigana nao kuanzia machweo ya jua hadi kesho yake jioni, na hakuna yeyote miongoni mwao aliyetoroka, isipokuwa vijana wanaume 400 waliopanda ngamia na kutoroka.
Esther 3:1Baada ya matukio haya, Mfalme Ahasuero alimheshimu Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, akampandisha na kumpa kiti chake cha heshima cha juu sana kuliko wakuu wengine wote.