Proverbs 10:9
Mtu mwadilifu hutembea salama, 2 lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
He that walketh uprightly walketh surely: but he that perverteth his ways shall be known.
In Context
8Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, 2 lakini mpumbavu apayukaye huangamia. 1
10Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, 2 naye mpumbavu apayukaye huangamia. 1
Cross References
Genesis 17:1Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; + 17:1 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu.
Psalms 23:4Hata kama nikipita katikati 2 ya bonde la uvuli wa mauti, 1 sitaogopa mabaya, 2 kwa maana wewe upo pamoja nami; 1 fimbo yako na mkongojo wako 2 vyanifariji. 1
Psalms 26:11Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; 2 nikomboe na unihurumie. 1
Proverbs 3:23Kisha utaenda katika njia yako salama, 2 wala mguu wako hautajikwaa; 1
Proverbs 28:1Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, 2 bali wenye haki ni wajasiri kama simba. 1
Isaiah 33:15Yeye aendaye kwa uadilifu 2 na kusema lililo haki, 1 yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma 2 na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, 1 yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, 2 na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu: 1