Proverbs 15:27
Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, 2 bali yeye achukiaye rushwa ataishi. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
He that is greedy of gain troubleth his own house; but he that hateth gifts shall live.
In Context
26Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu, 2 bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. 1
28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake, 2 bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. 1
Cross References
Exodus 18:21Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.
Deuteronomy 7:26Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.
Joshua 6:18Lakini mjiepushe na vitu vilivyowekwa wakfu, msije mkachukua chochote katika hivyo, msije mkajiletea maangamizi katika maskani ya Israeli na kuiletea taabu.
Joshua 7:24Basi Yoshua, pamoja na Israeli yote, wakamchukua Akani mwana wa Zera, pamoja na ile fedha, lile joho, ile kabari ya dhahabu, wanawe na binti zake, ngʼombe, punda na kondoo wake, hema yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta katika Bonde la Akori.
1 Samuel 8:3Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.
2 Kings 5:27Ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Elisha, mwenye ukoma, mweupe kama theluji.