Proverbs 16:6
Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; 2 kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
By mercy and truth iniquity is purged: and by the fear of the LORD men depart from evil.
In Context
7Njia za mtu zinapompendeza Bwana, 2 huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. 1
Cross References
Genesis 20:11Abrahamu akajibu, “Niliwaza kwamba, ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa sababu ya mke wangu.’
Leviticus 25:17Mmoja asimpunje mwingine, bali utamcha Mungu wako. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
Nehemiah 5:9Basi nikaendelea kusema, “Mnachokifanya si sawa. Je, haikuwapasa kutembea katika hofu ya Mungu wetu ili tuepukane na shutuma za adui zetu wasioamini?
Job 1:1Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.
Psalms 85:10Upendo na uaminifu hukutana pamoja, 2 haki na amani hubusiana. 1
Proverbs 8:13Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; 2 ninachukia kiburi na majivuno, 2 tabia mbaya na mazungumzo potovu. 1