Proverbs 28:12
Mwenye haki ashindapo, kuna furaha kubwa, 2 bali waovu watawalapo, watu hujificha. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
When righteous men do rejoice, there is great glory: but when the wicked rise, a man is hidden.
In Context
13Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, 2 bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. 1
Cross References
1 Samuel 24:11Tazama, baba yangu, ona kipande hiki cha joho lako mkononi mwangu! Nilikata upindo wa joho lako lakini sikukuua. Basi ujue na kutambua kuwa sina hatia ya kutenda mabaya wala ya kuasi. Wewe sijakukosea, lakini wewe unaniwinda mimi ili kuuondoa uhai wangu.
1 Kings 18:13Je, hukusikia, bwana wangu, nilifanya nini wakati Yezebeli alipokuwa akiua manabii wa Bwana? Niliwaficha manabii wa Bwana mia moja katika mapango mawili, hamsini katika kila moja, nami nikawapatia chakula na maji.
1 Chronicles 15:25Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.
1 Chronicles 29:20Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini Bwana Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za Bwana na mfalme. 1 Solomoni Akubalika Kuwa Mfalme
2 Chronicles 30:22Hezekia akazungumza akiwatia moyo Walawi wote, ambao walionyesha ustadi katika kumtumikia Bwana. Hivyo watu wakala chakula cha sikukuu kwa siku saba, wakitoa sadaka za amani na kumshukuru Bwana, Mungu wa baba zao.
Esther 8:16Kwa maana kwa Wayahudi ulikuwa wakati wa raha na furaha, shangwe na heshima.