Proverbs 28:15
Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, 2 ndivyo alivyo mtu mwovu atawalaye wanyonge. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
As a roaring lion, and a ranging bear; so is a wicked ruler over the poor people.
In Context
16Mtawala dhalimu hana akili, 2 bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu 2 atafurahia maisha marefu. 1
Cross References
Exodus 1:14Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.
1 Samuel 22:17Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Bwana, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.” Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa Bwana.
2 Kings 15:16Wakati ule, akianzia Tirsa, Menahemu alishambulia Tifsa na kila mtu ndani yake, na wale waliokuwa maeneo jirani, kwa sababu walikataa kufungua malango yao. Akaiangamiza Tifsa yote, na kuwapasua matumbo wanawake wote wenye mimba. 1 Menahemu Mfalme Wa Israeli
Esther 3:6Hata hivyo baada ya kujulishwa watu wa Mordekai ni akina nani, alibadili wazo la kumuua Mordekai peke yake. Badala yake Hamani alitafuta njia ya kuwaangamiza watu wote wa Mordekai, yaani, Wayahudi, walio katika ufalme wote wa Ahasuero.
Proverbs 19:12Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, 2 bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi. 1
Isaiah 14:5Bwana amevunja fimbo ya mwovu, 2 fimbo ya utawala ya watawala, 1