Ufunuo 1:13
na katikati ya vile vinara vya taa, alikuwamo mtu kama Mwana wa Adamu, akiwa amevaa joho refu, na mkanda wa dhahabu ukiwa umefungwa kifuani mwake.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 39:5Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi ulifanana nacho: ulikuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao ulitengenezwa kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Isaiah 11:5Haki itakuwa mkanda wake 2 na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake. 1
Daniel 7:9“Nilipoendelea kutazama, 1 “viti vya enzi vikawekwa, 2 naye Mzee wa Siku akaketi. 1 Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji; 2 nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu. 1 Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto, 2 nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto. 1
Daniel 10:5nikatazama juu, na mbele yangu alikuwepo mtu aliyevaa mavazi ya kitani na mshipi wa dhahabu safi kutoka ufazi kiunoni mwake.
Philippians 2:7bali alijifanya si kitu, 2 akachukua hali hasa na mtumwa, 2 naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu. 1
Hebrews 4:15Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo: lakini yeye hakutenda dhambi.