Romans 12:16
Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.
17Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote.
Cross References
Job 31:13“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, 2 walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu, 1
Psalms 131:1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, 2 macho yangu hayajivuni; 1 sijishughulishi na mambo makuu kunizidi 2 wala mambo ya ajabu mno kwangu. 1
Proverbs 17:5Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; 2 yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa. 1
Proverbs 19:17Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, 2 naye atamtuza kwa aliyotenda. 1
Proverbs 26:12Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima 2 machoni pake mwenyewe? 2 Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake. 1
Jeremiah 32:39Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao.