Romans 8:5
Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
6Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani.
Cross References
John 3:6Mwili huzaa mwili, lakini Roho huzaa roho.
Romans 8:9Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu yeyote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
1 Corinthians 2:14Mtu ambaye hana Roho hawezi kupokea mambo yatokayo kwa Roho wa Mungu, kwa kuwa ni upuzi kwake, naye hawezi kuyaelewa kwa sababu hayo yanaeleweka tu kwa upambanuzi wa rohoni.
2 Corinthians 10:3Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.
Ephesians 5:9(kwa kuwa tunda la nuru hupatikana katika wema wote, haki na kweli),
Colossians 3:1Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo alikoketi mkono wa kuume wa Mungu.