Zekaria 1:11
Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa Bwana, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 68:17Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu, 2 na maelfu ya maelfu; 1 Bwana amekuja kutoka Sinai 2 hadi katika patakatifu pake. 1
Isaiah 14:7Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani, 2 wanabubujika kwa kuimba. 1
Zechariah 1:8Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.
Zechariah 1:15lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’
Matthew 13:41Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote.
Matthew 24:30“Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu.