Zekaria 1:12
Kisha malaika wa Bwana akasema, “ Bwana Mwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
13Kwa hiyo Bwana akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami.
Cross References
2 Chronicles 36:21Nchi ikaendelea kufurahia pumziko lake la Sabato, wakati wote wa kufanywa kwake ukiwa ilipumzika mpaka ile miaka sabini ilipotimia katika kutimiza neno la Bwana lililonenwa na Yeremia. 1 Koreshi Atangaza Uhuru Kwa Waliokuwa Uhamishoni (Ezra 1:1-4)
Psalms 74:10Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? 2 Je, adui watalitukana jina lako milele? 1
Psalms 102:13Utainuka na kuihurumia Sayuni, 2 kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema; 2 wakati uliokubalika umewadia. 1
Isaiah 47:6Niliwakasirikia watu wangu 2 na kuaibisha urithi wangu; 1 niliwatia mikononi mwako, 2 nawe hukuwaonea huruma. 1 Hata juu ya wazee 2 uliweka nira nzito sana. 1
Isaiah 64:9Ee Bwana, usikasirike kupita kiasi, 2 usizikumbuke dhambi zetu milele. 1 Ee Bwana, utuangalie, twakuomba, 2 kwa kuwa sisi sote tu watu wako. 1
Jeremiah 25:11Nchi hii yote itakuwa ukiwa na isiyofaa kitu, nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.”