Zekaria 11:16
Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
15Kisha Bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu.
Cross References
Genesis 33:13Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ngʼombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa.
Isaiah 40:11Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo: 2 Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake 1 na kuwachukua karibu na moyo wake, 2 huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao. 1
Jeremiah 23:22Lakini kama wangesimama barazani mwangu, 2 wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu, 1 nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya 2 na kutoka matendo yao maovu.” 1
Ezekiel 34:10Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na wachungaji nami nitawadai kondoo zangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kwenye kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo zangu kutoka kwenye vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao.
Ezekiel 34:21Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu mpaka wakawafukuza,
Matthew 23:2“Walimu wa sheria na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Mose,