Zekaria 7:12
Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo Bwana Mwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote alikasirika sana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
11“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.
Cross References
Exodus 7:13Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amesema. 1 Pigo La Kwanza: Damu
Nehemiah 9:29“Ukawaonya warudi katika sheria yako, lakini wakawa na kiburi na hawakutii amri zako. Wakatenda dhambi dhidi ya maagizo yako ambayo kwayo mtu ataishi kama akiyatii. Kwa ukaidi wakakugeuzia kisogo, wakawa na shingo ngumu na wakakataa kusikiliza.
Psalms 50:17Unachukia mafundisho yangu 2 na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. 1
Isaiah 48:4Kwa kuwa nalijua jinsi ulivyokuwa mkaidi; 2 mishipa ya shingo yako ilikuwa chuma, 2 kipaji chako cha uso kilikuwa shaba. 1
Jeremiah 5:3Ee Bwana, je, macho yako hayaitafuti kweli? 2 Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu, 2 uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo. 1 Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe 2 nao walikataa kutubu. 1
Jeremiah 17:1“Dhambi ya Yuda imechorwa kwa kalamu ya chuma, 2 imeandikwa kwa ncha ya almasi, 1 kwenye vibao vya mioyo yao 2 na kwenye pembe za madhabahu zao. 1