1 Samweli 2:10
wale wampingao Bwana 2 wataharibiwa kabisa. 1 Atapiga radi dhidi yao kutoka mbinguni; 2 Bwana ataihukumu miisho ya dunia. 1 “Atampa nguvu mfalme wake, 2 na kuitukuza pembe 2 ya mpakwa mafuta wake.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 15:6“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana 2 ulitukuka kwa uweza. 1 Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, 2 ukamponda adui. 1
1 Samuel 7:10Samweli alipokuwa anatoa hiyo dhabihu ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu ili kupigana vita na Israeli. Lakini siku ile Bwana alinguruma kwa ngurumo kubwa dhidi ya Wafilisti na kuwafanya wafadhaike na kutetemeka hivi kwamba walikimbizwa mbele ya Waisraeli.
1 Samuel 12:13Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni, Bwana amemweka mfalme juu yenu.
1 Samuel 12:18Kisha Samweli akamwomba Bwana, na siku ile ile Bwana akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana Bwana na Samweli.
1 Samuel 16:1Bwana akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli mpaka lini, maadamu nimemkataa asiendelee kuwa mfalme juu ya Israeli? Jaza pembe yako mafuta, ushike njia uende; ninakutuma kwa Yese huko Bethlehemu. Nimemchagua mmoja wa wanawe kuwa mfalme.”
2 Samuel 7:13Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.