The Bible Software
bible.software2 Samuel2 Samuel 21 › 2 Samuel 21:16

2 Samuel 21:16

Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai, + 21:16 Yaani majitu. ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli 300 za shaba, + 21:16 Shekeli 300 za shaba ni sawa na kilo 3.5. alikuwa amejifunga upanga mpya, naye alisema angemuua Daudi.

Biblia (Kiswahili)

In The King James Version

And Ishbi-benob, which was of the sons of the giant, the weight of whose spear weighed three hundred shekels of brass in weight, he being girded with a new sword, thought to have slain David.

In Context

15Kwa mara nyingine tena kulikuwa na vita kati ya Wafilisti na Israeli. Daudi akashuka pamoja na watu wake ili kupigana dhidi ya Wafilisti, naye akawa amechoka sana.

17Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumuua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutakwenda tena nasi vitani, ili kwamba taa ya Israeli isije ikazimwa.”

Read all of 2 Samuel 21

Cross References

Genesis 14:5Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,

Deuteronomy 1:28Twende wapi? Ndugu zetu wametufanya kufa moyo. Wanasema, ‘Watu wa huko wana nguvu zaidi na ni warefu kuliko sisi tulivyo; miji ni mikubwa, yenye kuta zilizofika juu angani. Zaidi ya hayo, tumewaona Waanaki huko.’ ”

Deuteronomy 2:11Kama walivyokuwa Waanaki, hao pia walikuwa kama Warefai, lakini Wamoabu waliwaita Waemi.

Deuteronomy 3:11(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa + 3:11 Dhiraa tisa ni sawa na mita 4. na upana wa dhiraa nne. + 3:11 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.) 1 Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani (Hesabu 32:1-42)

Joshua 11:22Hawakubaki Waanaki wowote katika nchi ya Israeli, ila tu katika nchi ya Gaza, Gathi na Ashdodi.

1 Samuel 17:7Mpini wa huo mkuki ulikuwa kama mti wa mfumaji, na ncha ya chuma yake ilikuwa na uzito wa shekeli mia sita. + 17:7 Shekeli 600 ni sawa na kilo 7. Mbeba ngao wake alitangulia mbele yake.

This Verse In Other Editions

King James VersionBíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)Библия (Русский)聖經 (中文)성경 (한국어)الكتاب المقدس (العربية)बाइबल (हिन्दी)Bibbia Diodati (Italiano)Alkitab (Bahasa Indonesia)Kinh Thánh (Tiếng Việt)Biblia Cornilescu (Română)

Study 2 Samuel 21:16

Matthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)
← 2 Samuel 21:152 Samuel 212 Samuel 21:17 →