Genesis 14:5
Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
6na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa.
Cross References
Genesis 15:20Wahiti, Waperizi, Warefai,
Deuteronomy 2:10(Waemi walikuwa wakiishi huko hapo zamani, watu wenye nguvu na wengi, warefu kama Waanaki.
Deuteronomy 3:11(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa + 3:11 Dhiraa tisa ni sawa na mita 4. na upana wa dhiraa nne. + 3:11 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.) 1 Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani (Hesabu 32:1-42)
Deuteronomy 3:22Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”
Joshua 13:12yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao.
Joshua 13:31nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo.