2 Samweli 23:16
Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 35:14Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake.
1 Samuel 7:6Walipokwisha kukutanika huko Mispa, walichota maji na kuyamimina mbele za Bwana. Siku hiyo walifunga na wakaungama, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi ya Bwana.” Naye Samweli alikuwa kiongozi + 7:6 Kiongozi hapa maana yake mwamuzi. wa Israeli huko Mispa.
2 Samuel 23:9Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai, + 23:9 Dodai tafsiri nyingine zinamwita Dodo. Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,
Lamentations 2:19Inuka, lia usiku, 2 zamu za usiku zianzapo; 1 mimina moyo wako kama maji 2 mbele za Bwana. 1 Mwinulie yeye mikono yako 2 kwa ajili ya maisha ya watoto wako, 1 ambao wanazimia kwa njaa 2 kwenye kila mwanzo wa barabara. 1
Romans 5:7Hakika, ni vigumu mtu yeyote kufa kwa ajili ya mwenye haki, ingawa inawezekana mtu akathubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.
Philippians 2:17Lakini hata kama nikimiminwa kama sadaka ya kinywaji kwenye dhabihu na huduma itokayo katika imani yenu, mimi ninafurahi na kushangilia pamoja nanyi nyote.