Acts 16:31
Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
And they said, Believe on the Lord Jesus Christ, and thou shalt be saved, and thy house.
In Context
30Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?”
32Wakamwambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake.
Cross References
Genesis 18:19Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”
Jeremiah 32:39Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao.
Mark 16:16Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini yeyote asiyeamini atahukumiwa.
John 3:15Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.
John 6:40Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.”
John 7:37Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Yesu akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.